Your browser doesn’t support HTML5
Kamishna wa umoja wa ulaya anayeshughulikia masuala ya uhamiaji alionya jana kuwa mfumo wa uhamiaji wa kanda hiyo uko hatarini kuvunjika.
Akizungumza baada ya mkutano juu ya uhamiaji huko Brussels, kamishna wa ulaya kuhusu masuala ya uhamiaji Dimitris Avrampoulos, alionya wanachama wengineo wa umoja wa Ulaya kuwa wana mda wa wiki moja tu kupiga hatuwa juu ya mzozo huo Kabla ya mkutano na Uturuki hapo March 7.
Bw. Avrampoulos alisema kuwa, katika siku 10 zijazo, tutahitaji kuwa na matokeo mahsusi. Bila hivyo, kuna hatari, ya mfumo mzima kuvunjika.
Mkutano huo unalenga kutatuwa mgawanyiko mkubwa uliopo miongoni mwa wanachama wa nchi za umoja wa Ulaya juu ya kushughulikia wimbi kubwa la wahamiaji. Ugiriki ulimwita nyumbani balozi wake kwa Austria, baada ya Vienna kufanya mkutano na matiafa ya Balkan Jumatano, na ambapo maafisa wa Ugiriki hawakualikwa.
Wale walohudhuria ikiwa ni pamoja na wanachama wengine ambao hawatoki umoja wa Ulaya, walikubaliana juu ya vikwazo vilokubaliwa na wote, vya kupunguza watu wanaotafuta hifadhi wanaofika mipakani mwao. Hilo linaiacha Ugiriki, ambayo mara nyingi ndio kiiingilio cha kwanza kwawatafuta hifadhi, na tatizo linaloongezeka la wahamiaji. Athens imetishia kuzuia uwamuzi wa mbeleni wa umoja wa ulaya kuhusu wahamiaji, iwapo wanachama wa umoja huo, hawatokubali pendekezo la kugawana dhamana ya wahamiaji.
Akizungumza kando ya mkutano wa Brussels, kamishna wa wakimbizi wa umoja mataifa Fillipo Grandi anasema watu wengi wanaotafuta hifadhi wengi wanaowasili Ugiriki ni wakimbizi na sio wahamiaji wa kiuchumi.
Bw. Grandi alisema kuwa wamejadili na serikali ya Ugirikii jinsi ya kushughulikia uwezekano wa ongezeko la wakimbizi ambao wanabidi kubaki Ugiriki kwa sababu hawana sehemu nyingine ya kwenda. Lakini hilo litahitaji kazi nyingi na raslimali ziada.
Pia kuna ongezeko la mivutano kuhusu uhamiaji kwengineko vilevile, ikiwa ni pamoja na baina ya Ubelgiji na Ufaransa. Ubelgiji ilianza kuweka ukaguzi wa mipakani wiki hii ili kupunguza wahamiaji wanaoingia kutoka mji wa Ufaransa wa Calais, ambako hakimu mmoja huko alipitisha amri ya kuhamishwa kwa kambi ya wahamiaji.
Zaidi ya watafuta hifadhi millioni moja walikimbilia Ulaya mwaka jana, na zaidi ya laki moja wamewasili mwaka huu hadi sasa. Wataalam wanaonya kuwa hali ya hewa inapopata ujoto , basi idadi hio itaongezeka.