Katika mkutano wa pamoja, EU na China zimesema mabadiliko ya hali ya hewa na nishati safi “itakuwa ni nguzo yao muhimu” katika ushirikiano wao.
Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk amesema juhudi za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa zitaendelea, bila ya kujali kuwepo au kutokuwepo kwa Marekani:
“Leo, China na EU umeonyesha mshikamano wao kwa kushirikiana na kizazi kijacho na majukumu ya kusimamia dunia yote,” amesema. “Tunaamini kuwa uamuzi uliofanywa jana ni kosa kubwa.”
Waziri mkuu wa China Li Keqiang, akiwa Brussels kwa ajili ya mkutano wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na China, amesema ni jambo la muhimu kwa mahusiano ya China na EU kuimarishwa zaidi.
“Tunaamini kuwa kumekuwa na mabadiliko katika medani za kimataifa, na kutaendelea kuwepo mashaka na sababu zakutuyumbisha,” amesema. “Hili linatutaka tuongeze juhudi zetu ilikutatua mambo haya yanayotukabili.”