Ethiopia Jumatatu imeeleza kutofurahishwa na hatua ya Marekani ya kurejesha ushuru kwenye bidhaa zake zinaoingia Marekani.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, taarifa kutoka wizara ya biashara ya Ethiopia imelalamikia hatua ya Decemba 23 ya utawala wa Biden ya kuondoa faida kwa Ethiopia kupitia mkataba wa fursa ya maendeleo kwa Afrika maarufu kama AGOA, kama njia ya kutoridhishwa na mapigano yanayoendelea kwenye mkoa wa Tigray.
Serikali ya Ethiopia imesikitishwa juu ya uamuzi wa Marekani wa kuiondoa kunufaika na mpango wa AGOA, wizara imesema wakati ikiomba Marekani kufikiria uamuzi wake.
Marekani ilichukua hatua hiyo licha ya maombi kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Marekani pamoja na makundi ya wanaharakati, wakiuomba utawala wa Biden kutoa muda zaidi ili nchi hiyo ipate furs aya kutekeleza matakwa ya marekani.