Serikali ya Ethiopia imelaumu hasimu wake Misri kwa kuunga waasi mkono na kusababisha Addis Ababa kutangaza hali ya dharura siku ya Jumapili.
Zaidi ya watu 50 waliuwawa baada ya maafisa wa usalama kufiatulia waandamanaji risasi wakati wa sherehe za kidini zilizokuwa zikufanyika kwenye eneo la Bishoftu lililoko kusini mashariki mwa mji mkuu.
Tukio hilo lilisababisha maandamano zaidi katika eneo la Oromia yaliopelekea kuchomwa kwa mashamba, viwanda na majengo ya Serikali.
Msemaji wa serikali Getachew Reda, amesema Jumatatu kuwa hali ya tahadhari ya miezi sita itatoa nafasi kwa Serikali kukabiliana na kundi la Oromo Liberation Front lililopanga mashambulizi katika eneo la Oromia.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema takriban watu 400 wameuwawa kwenye maandamano dhidi ya serikali katika kipindi cha mwaka uliopita.