UN yaindolea vikwazo vya silaha Eritrea

Viongozi wa Djibouti and Eritrea.

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, Jumatano lillipiga kura kwa kauli moja ya kuiondolea Serikali ya Eritrea vikwazo vya kutouziwa silaha, ilivyowekewa takriban mwongo mmoja uliopita.

Hatua hiyo ilijiri baada ya nchi hiyo kuimarisha uhusiano wake na Ethiopia na Djibouti katika siku za hivi karibuni.

Kufuatia kura hiyo, Umoja wa Mataifa unazitaka Eritrea na Djibouti kuchukua hatua za haraka kuimarisha Zaidi uhusiano wao na kusuluhisha migogoro ya mpakani.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres ametakiwa kuripoti kwa baraza la usalama la umoja huo ifikapo februari 15 kuhusu hatua zitakazokuwa zimechukuliwa na Eritrea kuimarisha uhusiano na majirani wake na atakuwa akiwasilisha ripoti kama hiyo kila baada ya miezi sita.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa lajadili vikwazo vya Eritrea. Jumatano 14, 2018.

Vikwazo dhidi ya Eritrea na maafisa wa ngazi ya juu serikali viliwekwa mwaka 2009 baada ya wataalam wa Umoja wa mataifa kuishutumu Eritrea kwamba ilikuwa inayasaidia makundi ya wapiganaji nchini Somalia.

Eritrea hata hivyo, imekuwa ikipinga vikali na kukanusha madai hayo.