Elon Musk alisema Jumapili kwamba anapanga kubadilisha nembo ya Twitter kuwa “X” kutoka nembo ya ndege ikiashiria kwamba yatakuwa mabadiliko makubwa ya hivi karibuni tangu aliponunua jukwaa la mtandao wa kijamii kwa dola 44 bilioni mwaka 2022.
Katika mfululizo wa machapisho kwenye akaunti yake ya Twitter kuanzia saa sita usiku kuamkia leo Jumapili mmiliki huyo wa Twitter alisema kuwa anatarajia kufanya mabadiliko ya haraka duniani kote ikiwezekana Jumatatu. "Na hivi karibuni tutabadilisha chapa ya Twitter na kwa polepole tutaondoa ndege wote", Musk aliandika kwenye akaunti yake.
Mapema mwezi huu Musk aliweka masharti mapya katika uwanja wake wa kidijitali hatua ambayo ilikosolewa vikali kwamba inaweza kuwafukuza watoa matangazo na kudhoofisha ushawishi wake wa kitamaduni unaovuma wakati huu.