Rais Kenyatta azindua mradi wa kusambaza umeme Mombasa.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta ambae bado yuko kwenye ziara ya maendeleo katika Pwani ya Mombasa amezindua mradi mkubwa uliopewa jina Mwangaza Mitaani, unaonuia kusamabza nguvu za umeme kote nchini hadi mashinani, na kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata huduma hiyo kufikia mwaka wa 2020.

Your browser doesn’t support HTML5

Umeme Mombasa.

Uhuru amesema awamu ya kwanza ya mradi huo tayari imefikisha umeme kwa miji 51, ambako hali ya usalama inatarajiwa kuimarika na pia kuongeza nafasi za ajira kwa vijana.

Mradi huo umeongeza kiwango cha umeme unaotumika kote nchini kutoka megawati 615 iliovukuwa mwaka 2013 hadi megawati 2282 zinazotumika sasa. Kampuni ya kutoa umeme nchini KPLC pia imeongeza idadi ya wateja wake kutoka milioni mbili hadi milioni 4 katika kipindi hicho.