Nigeria imeongeza muda wa kupiga kura hadi Jumapili kufuatia matatizo kadhaa kutkana na mamillioni ya watu kujitokeza kupiga kura Jumamosi katika uchaguzi wa rais na bunge la nchi hiyo.
Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa uchaguzi utaendelea Jumapili katika maeneo ambako mashine za kupigia kura BVR hazikufanya kazi vizuri, alisema msemaji wa tume, Kayode Idowu. Maeneo ambako uchaguzi utaendelea Jumapili ni pamoja na Lagos, mji mkubwa kuliko yote nchini Nigeria.
Katika maeneo mengine hesabu ya kura zilizopigwa tayari umeanza, alisema msemaji huyo wa tume.
Karibu watu millioni 60 wana kadi za kupigia kura kuamua nani atakuwa rais ajaye wa Nigeria baina ya Rais Goodluck Jonathan na mpinzani wake kiongozi wa zamani wa kijeshi Muhammadu Buhari.