Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imelaani vikali kuzuka kwa mapigano Ijumaa huko Guinea-Bissau, ambapo hali imerejea kuwa shwari siku ya Jumamosi.
Mapambano kati ya walinzi wa kitaifa na kikosi maalum cha walinzi wa rais yalizuka Alhamisi usiku katika mji mkuu Bissau, na kusababisha vifo vya watu wawili.
ECOWAS inalaani vikali ghasia na majaribio yote ya kuvuruga utaratibu wa kikatiba na utawala wa sheria nchini Guinea-Bissau, jumuiya hiyo yenye makao yake makuu mjini Abuja lilisema katika taarifa yake.
ECOWAS imetoa wito zaidi wa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa wahusika wa tukio hilo kwa mujibu wa sheria.