Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika Arusha

Rais Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwenye picha ya awali. (kushoto kulia)

Mkutano wa viongozi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika Jumatano katika makao yake makuu yalioko kwenye mji wa Arusha, Tanzania. Baadhi ya viongozi wa kieneo walikuwa tayari wameanza kufika mapema kwa madhumuni ya kujadili maswala muhimu ya kieneo.

Your browser doesn’t support HTML5

EA- SUMMIT

Kwa wakati fulani, ilisemekana kuwa Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi angeshiriki lakini baadaye ikabainika kuwa alimtuma makamu wa Rais kumuakulisha. Rais Yoweri Museveni wa Uganda ni miongoni mwa wale waliofika kwanza akilakiwa na mwenyeji wake Rais John Magufuli wa Tanzania.