Mapinduzi nchini Niger yanaweza kuwa na athari mbaya kwa Umoja wa Mataifa kuondoa operesheni zake za muongo mmoja za kulinda amani katika nchi jirani ya Mali, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alisema Alhamisi.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi uliopita lilihitimisha operesheni zake nchini Mali baada ya utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuwataka ghafla wanajeshi 13,000 kuondoka katika hatua ambayo Marekani ilisema imesukumwa na kundi la mamluki la Wagner la Russia.
Chad ndio mchangiaji mkubwa katika operesheni hiyo ikiwa na takriban wanajeshi 1,400 nchini Mali lakini mapinduzi ya Niger siku ya Jumatano yanaweza kufanya iwe vigumu kwao kurejea nyumbani.
Baraza la Usalama limeitaka tume ya kulinda amani kulenga kukamilisha kujiondoa mwishoni mwa mwaka huu