Majaribio hayo ni katika harakati za kudhibiti ugonjwa huo unaoendelea kuenea eneo la mashariki mwa DRC na kusababisha maafa.
Wizara ya afya imesema wagonjwa 10 waliopewa dawa aina MAB 114 tangu Agosti 11 wanaendelea vizuri na matibabu hayo.
Kumekuwapo wagonjwa sita wapya waliokutikana na virusi vya Ebola na vifo vinne vilivyo ripotiwa na wizara ya Afya, na hivyo imepelekea idadi ya vifo 59 na wagonjwa kufikia 75 tangu mwezi Julai.
Wafanyakazi wa afya zaidi ya elfu moja na mia sita pamoja na watu waliokuwa na mawasaliano na wagonjwa wa Ebola walipewa chanjo dhidi ya Ebola iliolipuka mapema mwezi Agosti kaskazini magharibi mwa DRC.