DRC: Waziri ana azma kufuta hati ya kampuni ya EGC ya kuhodhi uchimbaji

Vipande vya madini ya cobalt vikitengenezwa katika kiwanda cha Lubumbashi, Congo, on Feb. 16, 2018, kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.

Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Antoniette N’samba Kalambayi anataka kufuta amri ya umiliki iliyotolewa kwa kampuni ya Generale Du Combat yenye mkataba na serikali kwa madini Ya cobalt  nchini humo, shirika la habari la ROITA limesema siku ya Jumatano.

EGC iliundwa kwa ajili ya kununua, kutengeneza na kutafuta soko la madini hayo kwa amri ya serikali ya mwaka 2019 na ilizinduliwa rasmi Machi mwaka jana, lakini hadi sasa haijanunua aina yoyote ya madini ya cobalt.

Wachimbaji ambao wanachimba madini kwa njia zisizo za kawaida ni chanzo kikubwa duniani cha bidhaa za chuma zinazotumika katika betri za magari ya umeme baada ya migodi ya Congo.

Kitengo cha serikali cha uchimbaji madini katika kampuni ya Gecamines na operesheni za EGC zimekwama kutokana na mizozo ya ndani kati ya idara za serikali, mabadiliko ya uongozi katika Gecamines na changamoto ya kupata fursa katika maeneo ya uchimbaji kwa ajili ya kununua.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu EGC Kalambayi alisema, “ nisingesema ninaunga mkono au kupinga lakini jambo moja la uhakika tulitoa umiliki binafsi kwa kampuni ya EGC na huo ni ukiukwaji wa sheria za congo.”

Waziri huyo wa madini hataki kuivunja EGC lakini kufuta umiliki wa kisheria ilionao, amesema ili makampuni yote yapate fursa ya kuwania ununuzi wa machimbo ya cobalt.

Hata hivyo EGC haikujibu haraka barua pepe iliyoandikiwa kwa ajili ya kutoa maoni yake kufuatia maelezo ya waziri huyo.