Katika taarifa ya maandishi, mawakili hao wametaka kampuni ya Apple kujibu maswali kuhusu namna inavyopata madini kutoka Congo, na kusema wanathathmini kuichukulia hatua za kisheria.
Kampuni ya Apple haijajibu madai hayo.
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imekumbwa na vita tangu miaka ya 1990, hasa mashariki mwa nchi hiyo, ambapo kuna makundi kadhaa yenye silaha, baadhi yanaungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda.
Mawakili wa Congo waliandikia mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook mnamo April 22, na kuzua tetezi kadhaa kuhusu madini ya Congo.
Waliandikia pia washirika wa Apple nchini Ufaransa wakitaka majibu ndani ya muda wa wiki tatu.
Mawakili hao wa Amsterdam na washirika wao, wamekuwa wakifanya uchunguzi kuhusu madai ya madini ya Congo kusafirishwa kwa njia ya magendo kupitia Rwanda, Uganda na Burundi.