Takriban watu 50, inasemekana wamekufa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo asubuhi ya kuamkia Alhamisi kutokana na ajali ya trenikusini mashariki mwa nchi hiyo, kulingana na ujumbe uliotumwa kupitia tweeter na Waziri wa Maswala ya kibinadamu, Steve Mbiyaki.
Kulingana na Mbiyaki, aliongeza kuwa takriban watu ishirini na watatu walijeruhiwa. Hata hivyo Gavana wa jimbo la Tanganyika ilipotokea ajali hiyo Zoe Kabila alitoa idadi ya watu 10 waliokufa na wengine 30 kujeruhiwa.
Baadaye akizungumza na shirika la habari la Reuters, Waziri Mbiyaki alisema kuwa anaelewa tofauti ilioko kwenye idadi iliotolewa ya maafa, lakini wanaendelea kutadhmini idadi kamili, wakati shughuli za uokozi zikiendelea.
Muda mfupi baada ya ajali hiyo, Harison Kamau wa VOA alizungumza na Kahozi Kosha akiwa Lubumbashi ambaye alianza kwa kueleza aina ya treni iliohusika kwenye ajali hiyo.
Your browser doesn’t support HTML5