Mkuu huyo ametaja jambo hilo kutokea katika miezi ijayo na mapema mwaka ujao wakati misimu miwili zaidi ya kiangazi ambayo inatarajiwa kuingilia kati ukame wa kihistoria ambao umelikumba taifa hilo la pembe ya Afrika.
Martin Griffiths alisema katika mkutano kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Somalia Mogadishu, kwamba ripoti mpya kutoka kwa jopo lenye mamlaka la wataalamu huru inasema kutakuwa na baa la njaa nchini Somalia kati ya Oktoba na Disemba ikiwa hawatafanikiwa kuizuia na kuiepuka kama ilivyokuwa mwaka 2016 na mwaka 2017.