Dhoruba yazidi kuleta maafa Ugiriki

Picha za madhara ya kimbunga nchini Ugiriki.

Serekali ya visiwa vya Ugiriki vya Rhodes, na Lemnos, imetangaza hali ya dharura Jumatatu, baada ya dhoruba kukumba visiwa hivyo na kusababisha vifo vya watu wawili na kufanya uharibifu mkubwa.

Timu ya uokozi ilisaidia jeshi na idara nyingine za serekali kuokoa wakazi wengi wazee katika maeneo ya mafuriko, baada ya upepo na mvua kali mwishoni mwa wiki kupindua magari, kukata umeme na kuharibu barabara.

Wanaume wawili waliuwawa katika vijiji vilivyokubwa na mafuriko vya Lemnos, wakati dazeni ya watu wakiokolewa na kupelekwa kwenye hoteli za kisiwa cha bandari kuu.

Vassilis Kikilias, waziri wa dharura za vimbunga na ulinzi wa raia, ametoa mwito kwa wakazi katika maeneo yaliyo shambuliwa na kimbunga kufuata amri za kuondoka makwao ambazo zinatangazwa kwa tahadhari za simu.