Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi kutokana na dhoruba Trami nchini Ufilipino imevuka watu 100 huku serikai ikisema kwamba sehemu kubwa ya nchi imetengwa kutoka na mafuriko na watu wanahitaji kuokolewa.
Dhoruba Trami imepiga sehemu za kaskasini magharibi mwa Ufilipino jana Ijumaa, na kusababisha vifo vya watu 81 na 34 hawajulikani walipo katika katika moja ya visiwa vya Kusini Mashariki mwa Asia.
Dhoruba hiyo ni mbaya zaidi kuwahi kutokea humo mwaka huu.
Idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka.
Waokoaji wanaendelea na kuwatafuta manusura katika mji wa Talisay ulio karibu za ziwa, katika jimbo la Batangas.