Dhana ya mabadiliko ya kisiasa Marekani kuwa ni udhaifu yapingwa

Wanadiplomasia wa Marekani na maafisa wa kijeshi wamepinga kwamba wasiwasi wa mabadiliko ya hivi karibuni na ghafla ya mazingira ya kisiasa ya Marekani kuwa ni ishara ya udhaifu, wakiwaonya wapinzani wa Marekani Alhamisi kutojaribu kutafuta kunufaika kwa hali yoyote ile.

“Wanapaswa kufikiria tena,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Matthew Miller, aliwaeleza waandishi wa habari.

“Wanapaswa kukemewa kwa dhana kwamba sisi si chochote ila kuzingatia changamoto za usalama wa kitaifa ambazo nchi inakabiliwa nazo,” aliongeza kusema.

Ndani ya Pentagon, maafisa wa kijeshi walisisitiza kwamba changamoto zozote ambazo maadui wa Marekani wanaweza kuzitumia, basi jeshi la Marekani liko tayari kuwakabili.