Darzeni ya watu Marekani wanahofiwa kufa kutokana na Kimbunga

Hali mbaya ya hewa iliyosababisha uharibifu ikiwemo jimbo la Tennessee, Marekani

Gavana wa jimbo la Kentucky, Andy Beshear alikiambia kituo cha televisheni cha WLKY kwamba takriban  watu 50 huenda wamefariki na kuongeza kuwa anatarajia idadi hiyo kuongezeka

Darzeni ya watu Marekani wanahofiwa kufa baada ya mfululizo wa vimbunga kutokea Ijumaa usiku katika majimbo kadhaa ya Marekani, na kusababisha uharibifu mkubwa kutokana na hali ya hewa inayotokea sana katika majira ya Spring.

Gavana wa jimbo la Kentucky, Andy Beshear alikiambia kituo cha televisheni cha WLKY kwamba takriban watu 50 huenda wamefariki na kuongeza kuwa anatarajia idadi hiyo kuongezeka. Beshear alitangaza hali ya dharura na ametoa wito kuwekwa walinzi wa kitaifa wa Kentucky na kupeleka polisi wa serikali ya jimbo.

Hali mbaya ya hewa katika jimbo la Kentucky, Disemba 11, 2021. (Foto: REUTERS/Cheney Orr)

Huko Edwardsville, polisi wa jimbo la Illinois, walisema katika taarifa kwenye Facebook kwamba hali mbaya ya hewa imesababisha tukio la kuporomoka kwa sehemu ya jengo kwenye ghala ya Amazon, na operesheni za uokoaji zinaendelea.

Kimbunga pia kilipiga nyumba ya kuhudumia wazee huko Monette, kaskazini mwa Arkansas, lakini kiwango cha majeruhi hakijafahamika mara moja. Maafisa walisema vimbunga vilihamia angalau kwenye majimbo matano ya Marekani, ya Arkansas, Illinois, Kentucky, Missouri na Tennessee.