Kamati ya afya ya bunge mjini Canbera imesema kwamba imepata taarifa kutoka vituo vya afya kwamba kuna idadi kubwa ya watu wanaotafuta huduma za kimatibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Ripoti zimeongeza kusema kwamba licha ya viwango vya maambukizi mapya kushuka nchini humo, athari za maambukizi zimeendelea kushuhudiwa miongoni mwa baadhi ya waliomabukizwa awali.
Ripoti ya utafiti ya Jumatano kutoka chuo kikuu cha kitaifa cha Australia inaonyesha kwamba kwa kila mtu mmoja kati ya watatu waliyowahi kupata maambukizi, ameendelea kuonyesha dalili za maambukizi kwa zaidi ya wiki tatu, ikiwa ishara ya kile kimetajwa kuwa maambukizi ya Covid ya muda mrefu. Miongoni mwa dalili ni pamoja na uchovu, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, maumivu ya misuli pamoja na kikohozi.