Bao la dakika za mwisho la kipindi cha kwanza la Mislav Orsic lilitosha kumaliza pambano hilo. Mabao ya mapema ndani ya dakika tisa za kwanza ambapo kwa upande wa Croatia Josko Gvardiol aliandika bao katika dakika ya 7.
Mabao hayo yalisababisha mtanange kuwa mkali, huku Achraf Dari akisawazisha bao la Morocco katika dakika ya 9.
Medali ya shaba inaweza kuwa si kitu zaidi ya faraja baada ya pande zote mbili kuvumilia kukatishwa tamaa katika nusu fainali, lakini Croatia na Morocco zilionekana kuwa na hamu ya kufanya marekebisho baada ya kushindwa na timu za Argentina na Ufaransa katika nusu fainali.
Katika mchezo mkali na wa kusisimua, Croatia walipata bao la pili kupitia kwa kazi nzuri ya Mislav Oršić katika dakika ya 42.
Morocco pamoja na kufungwalakini imeweka historia ya kuwa taifa la kwanza la Afrika kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Nafasi ya tatu ya Croatia ni ya mara ya pili katika Kombe la Dunia, baada ya kumaliza nafasi ya tatu mwaka 1998. Na huko nchini Russia miaka minne iliyopita Croatia ilimaliza katika nafasi ya pili.