CPJ yashinikiza DRC kumfutia mashtaka mwandishi wa habari

Waandishi wanaofanya kazi na CPJ walioko jela

Taasisi ya kuwahami waandishi CPJ inaitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kumwachia mara moja mhariri wa gazeti binafsi la La Percee aliyekamatwa Octoba 10 jijini Kinshasa.

Pia CPJ inaitaka serikali kumfutia kosa la jinai dhidi ya mhariri ambaye ni mwanamama kwa madai ya kuandika habari za kashfa.

Kiaku ameshtakiwa kwa kuchapisha makala mbili katika gazeti la La Percee Septemba 6 na 13 juu ya wafanyakazi wa benki kubwa iliyokuwa haijalipamishahara yao kwa zaidi ya miaka 10, athari za kutokulipwa kwa familia zao na madai ya misimamo isiyo kuwa na maana wa mameneja walioko madarakani hivi sasa ambao mpaka sasa wanadaiwa kulipa mishahara hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya kikundi kinacho fuatilia uhuru wa habari cha Observatoire pour la Liberté de la Presse en Afrique, Kiaku alikamatwa wakati wa jioni ya Octoba 10 akiwa njiani anaelekea nyumbani akitoka kazini na maafisa wa polisi Kinshasa baada ya hati ya kuamuru kukamatwa kwake kutolewa na hakimu wa mjini hapo.

Kiaku alishikiliwa usiku wote katika rumande ya Mahakama ya Amani Gombe, Kinshasa kabla ya kupelekwa katika ofisi ya mwendesha mashtaka kwa shtaka la uvunjaji heshima jana, wakili wake, Dieudone Mpoyo ameiambia CPJ..

Baada ya kuzuiliwa kwa siku moja nyingine katika rumande ya mahakama, alihamishwa Ijumaa kwenye jela ya Kinshasa, Mpoyo amesema. Kiaku hakuweza kulipa papo hapo dhamana ya dola za Marekani 1,000 zilizotakiwa na Mahakama, amesema.

Lowassa: wananchi wamejazwa hofu