Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na makamu wake Yemi Osibanjo wamekuwa watu wa kwanza kupatiwa chanjo ikiwa ni njia ya kuwahakikishia wananchi kuwa chanjo ndiyo kinga muafaka dhidi ya virusi vya corona.
Nigeria wiki iliyopita ilipokea chanjo ya Covid 19 ikiwa ni mwanzoni mwa awamu ya pili ya mapambano dhidi ya janga la virusi vya corona, huku kampeni ikiendelea kuelimisha raia kuhusu Covid na hatua za msingi za kuchukuliwa kuzuia na maambukizi.
Rais Buhari na makamu wake Osinbajo walikuwa wa kwanza kwenye orodha ya viongozi wa siasa Nigeria kupatiwa chanjo kama njia moja ya kushawishi wananchi kuchukua chanjo hiyo ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kujikinga na janga la Covid.
Mara baada ya kupatiwa chanjo Rais Buhari alitumia fursa kuwaomba raia wa nchi hiyo kufahamu vizuri umuhimu wa kupatiwa chanjo ili kujikinga na virusi vya corona kama yeye alivyofaya pamoja na makamu wake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Rais juu ya Covid 19, Boss Mustapha amesema hatua ya rais na makamu wake kupatiwa chanjo inaonyesha dhahiri kuwa uongozi wa Nigeria una imani kwa chanjo zilizoagizwa kutoka nje na kwamba hazina madhara.
Awali katika Hospitali ya Taifa mjini Abuja madaktari wanao simamia matibabu kwa wagonjwa wa virusi vya corona walipatiwa chanjo. Cyprian Ngong ambaye alikuwa mnigeria wa kwanza kupatiwa chanjo dhidi ya Covid 19 amewataka wanigeria kufuata mfano wake wa kupatiwa chanjo.
Mwishoni mwa zoezi hilo la kutoa chanjo, Rais Buhari ametoa kwa makundi mbali mbali kujiunga katika kampeni za kuwashawishi wa Nigeria wengine kuchukua chanjo hiyo kwasababu ya usalama wao kiafya.
Ombi la Rais Buhari kwa waNigeria kujipatia chanjo dhidi ya Covid 19 ni kwasababu ya tabia ya kawaida ambayo wanigeria wengi wameonyesha hapo kabla dhidi ya utumiaji wa chanjo kutokana na Imani kwamba chanjo zinaathari mbaya dhidi ya afya haswa afya ya uzazi. Kwasasa, mpango wa kuwachanja madaktari na wafanyakazi wa afya unaendelea.
Imetayarishwa Na Mwandishi Wetu Collins Atohengbe, Lagos, Nigeria
I