Kamati ya kitaifa ya dharura kwa ajili ya COVID 19 imetoa taarifa hiyo kwenye twitter bila ya kutoa maelezo zaidi. Imesema mgonjwa anaendelea vizuri na anapewa huduma za afya zinazohitajika.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi wao wakisema iwapo virusi hivyo vitasambaa nchini Yemen, athari yake itakuwa janga kubwa, kwa sababu mfumo wa huduma za afya kwa nusu ya raia wote wa Yemen ni duni sana.
UN imeeleza kuwa taifa hilo linakabiliwa na uhaba wa vifaa muhimu vya matibabu, wataalam wa kutosha na uhaba wa vituo vya kutoa huduma.
Habari hiyo imefuatia taarifa ya sitisho la mapigano nchini kote kufuati wito wa UN ukizitaka pande zote hasimu duniani kusitisha mapigano ili kutoa fursa kwa misaada ya dharura kufikia nchi hizo kukabiliana na mlipuko wa corona.
Serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia illitangaza kusitisha operesheni za kijeshi katika kipindi cha wiki maili, lakini waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran walikuwa hawakubaliana na pendekezo hilo la serikali.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.