Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO, Alhamisi limezisihi nchi za Afrika kuandaa mipango ya kusambaza chanjo za COVID-19 kadri zitakavyopatikana.
Utafiti mpya wa WHO uligundua kuwa nchi nyingi za Kiafrika haziko tayari kwa kile kitakachokuwa harakati kubwa zaidi ya chanjo barani humo.
Kupanga na kuandaa mikakati kutafanikisha au kuharibu shughuli hii ambayo haijawahi kutokea, na tunahitaji uongozi na ushiriki kutoka ngazi za juu za serikali na mipango thabiti, ya kina ya uratibu wa kitaifa na mifumo iliyowekwa, Dk Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa kanda wa WHO wa Afrika, alinukuliwa akisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.
Wataalam walionya kwamba wakati maendeleo ya chanjo yanapaswa kusherehekewa, ni hatua ya kwanza tu katika kutolewa kwa mafanikio.
Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington Dc