Mpatanishi wa mazungumzo huko Comoros, mwakilishi wa Umoja wa Afrika Francisco Madeira amesema masharti yanao hitajika kwa majadiliano hayapo na hivyo hayawezi kuendelea.
Mwenyekiti wa mazungumzo spika wa zamani Abdallah Halifa, akizungumza baada ya siku tatau ya mzungumzo siku ya Ijuma amesma alilazimika kusitisha majadiliano kutokana na kutoelewana kwa wajumbe.
Mazungumzo yalipoanza wakjati muda wa mhula wa rais Sambi kumalizika hapo May 26, pande zote zilikubaliana kuanda uchaguzi hapo mwezi wa Novemba na kupunguza muda wa mhula wa magavana wa visiwa ili uchgauzi ufanyike kwa wakati mmoja.
Lakini baada ya siku tatu ya majadiliano rais Sambi alikutana na wawakilishi wa jumuia ya kimataifa na inaminika aliwambia hatoacha madaraka hadi mwezi May mwakani atakapotimiza miaka mitano kama ilivyoidhinishwa katika katiba mpya.
Akizungumza na Sauti ya Amerika, msemaji wa upinzani Ali Homadi Msaidie, amesema Sambi amefanya mapinduzi ya kikatiba na kwamba wanatafakari hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo. Amesema kiongozi huyo aliwambia wapatanishi wa kimataifa kwamba akiondoka madarakani hivi sasa huwenda hali ya uwasi wa kutaka kujitenga kwa kisiwa cha Nzwani ikazuka upya
Hivyo anasema anakwenda kinyume na msimamo wake wa awali wa kukubaliana na uvamizi wa Umoja wa Afrika kumondoa kiongozi aliyetaka kujitenga kwa Nzwani Mohamed Bakar.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Moroni Mohamed Mshangama ameiambia sauti ya Amerika kwamba hivi sasa rais Sambi anadharua uwamuzi wa mahakama ya katiba na kutojali wito wa jumia ya kimataifa kumtaka afikiye maridhiano na wapinzani kutayarisha uchaguzi.
Mapema mwezi May, mahakama ya katiba ya Comoros iliamua kwamba mhula wa Sambi unamalizika tarehe 26 May, lakini mahakama pia iliamua kwamba, kwa vile kiongozi huyo anaweza kubaki madarakani akiwa na madaraka ya mpito hadi kufanyika uchgauzi mpya kwa maridhiano na upinzani na wadau wote wanaohusika.
Hali hivi sasa ni ya wasi wasi katika visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi, hasa baada ya mandamano na ghasia wiki hii katika kisiwa kidogo cha Mwali, ambako wananchi wanadai ni zamu yao kuiongoza nchi hiyo.