Trump amkaribia Clinton kwa maoni ya umma

Donald Trump amkaribia Hillary Clinton kwenye uchunguzi wa maoni.

Mrepublican Donald Trump anaelekea kumkaribia mdemocrat Hillary Clinton katika ukusanyaji maoni ya umma kwa uchaguzi wa rais, ikiwa ni wiki tatu kabla ya mdahalo wao wa kwanza wa uso kwa uso.

Maoni kadhaa hapa Marekani yanaonyeshwa kuwa Clinton waziri wa zamani wa mambo ya nje, akiwa mbele ya Trump, ambaye anawania kwa mara ya kwanza nafasi ya kuchaguliwa.

Lakini amepunguza idadi ya uongozi wa Clinton kwa asilimia nne au chini ya hapo, ikiwa nusu ya mwanya uliokuwepo wiki chache zilizopita, hata wakati anaendelea kupunguza mwanayo huo katika majimbo kadhaa yenye ushindani mkali ambayo ndiyo yatabainisha matokeo ya uchaguzi wa novemba 8.

Wachambuzi kadhaa wa kisiasa bado wanabashiri Clinton atakuwa rais wa 45 wa marekani na mkuu wa kwanza wa majeshi mwanamke, baada ya rais barack obama kuondoka madarakani januari mwaka ujao.