Baada ya siku nne za mkutano mkuu wa cham,a cha Demiokratik uliofanyika mjini Philadelphiia, Pennsylvania, Marekjani, Bi Hillary Clinton, siku ya Alhamisi alikubali rasmi uteuzi wa chama chama hicho, kugombea kiti cha rais wa na akatoa wito kwa Wamarekani kuungana pamoja ili "kukabiliana na changamoto zinazotukumba."
Katika hotuba yake, Bi Clinton alwaambia waliohudhuria mkutano huo mkuu wa chama na taifa nzima kwa jumla, kuwa yeye ndiye anafaa kuwa kiongozi wa nchi hii baada ya rais Obama kuondoka mamlakani mwezi Januari mwaka ujao, na kutoa sababu kadhaa ambazo alisema kuwa zinaonyesha kwamba mpinzani wake kwa tikiti ya Reublican, Donald Trump, "hana ujuzi wala uwezo wa kuongoza Marekani."
Bi Clinton alikaribishwa kwenye ukumbi wa Wells Fargo mjini Philadelphia, jimbo la Pennslvynia, na bintiye, Chelsea Clinton, na kushangiliwa kwa muda na wajumbe waliokuwa wamesimama kwa heshima, kabla ya kuanza kutoa hotuba yake.
Baada ya Chelsea Clinton kutoa hotuba fupi, kanda ya video iliyoonyesa wasifu wa Bi Clinton ilichezwa, kabla ya mwanasiasa huyo kutembea hadi kenye jukwaa na kuanza kuzungumza.
Uteuzi huo wa Alhamisi ni wa Kihistoria kwa sababu ndiyo mara ya kwanza kwa chama kikuu cha Marekani kumteua mwanamke kugombea urais.
Kulingana na kampuni ya maoni ya Gallup, Bi Clinton, ambaye amekuwa mwanamke wa kwanza wa chama kikubwa cha Marekani kuteuliwa kama mgombea wa Urais, pia ndiye mwanamke anayependwa sana duniani kote.
Hata hivyo, wengi wa wapiga kura wa Marekani wamesema kupitia uchunguzi wa maoni kuwa hawamuamini, jambo ambalo limemfanya kushindana kwa karibu mno na mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump, huku kila mmoja akitaka kupata angalau muhula mmoja wa miaka minne katika Ikulu.
Clinton, mwenye umri wa miaka sitini na minane, alikuwa waziri wa mambo ya nje katika utawala wa rais Barack Obama kutoka mwaka wa 2009 hadi mwaka wa 2013. Siku ya Jumatano, Clinton na Obama walikuwa pamoja kwenye jukwaa hilo kwa muda mfupi, baada ya rais Obama kutoa hotuba ya kusisimua, na kumueleza Clinton kama mtu pekee aliyehetimu kuwa rais wa Marekani.