Chombo huru cha habari cha Russia, kimeandikisha vifo zaidi ya 50,000 miongoni mwao vikiwa vya wanajeshi wa Russia, toka uvamizi wake kamili kwa Ukraine, zaidi ya miaka miwili iliyopita, huku kikisema maelfu wengine wanaaminika wamekufa.
Mediazona ambayo inafuatilia vifo vya Russia, na BBC kutoka vyanzo vya wazi vya vifo hivyo, imesema katika taarifa zake za sasa wanajeshi 50,471 wa Russia, walipoteza maisha katika vita toka kuanza kwake Februari 2022.
Zaidi ya wanajeshi 85,000 wa Russia, wameuwawa kwa mujibu wa taarifa za idadi ya makazi na urithi kwa wanajeshi waliouawa ambazo zimeandikishwa kwa mujibu wa Mediazona.
Chombo hicho kiliandikwa kwamba “tunajua majina ya zaidi ya maafisa 3,300 wa jeshi na vikosi vingine vya usalama, 390 kati yao wana cheo cha luteni kanali na zaidi.