Maafisa nchini China wanasema,mwanamme mmoja aliyekuwa na milipuko iliyotengenezwa nyumbani, alijeruhi watu 3 katika eneo la ukaguzi la uwanja wa ndege wa Shanghai, katika juhudi za kujiuwa mwenyewe.
Mwanamume huyo ambaye hajatambuliwa aliondowa chupa zilokuwa na vifaa vya kulipuka kutoka kwenye mkoba wake kabla ya kurusha chupa moja katika eneo la Terminal Two kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pudong mjini Shanghai, maafisa wanasema.
Mwanamume huyo alitowa kisu, na kujikata shingo. Maafisa wanasema kuwa mwanamume huyo sasa yuko katika hali mahtuti hospitalini.
Lengo lake halikuwa bayana.
Waathirika wanne walijeruhiwa a vipande vya vigae na wanatibiwa hospitalini, hayo ni kwa mujib wa shirika la habari la China Xinhua.
Tukio hilo lilivuruga shughuli kwenye eneo la ukaguzi kwenye uwanja wa ndege, lakini baadae hali ilirejea kuwa ya kawaida.
Uwanja wa ndege ulikuwa umejaa watu waliokuwa wanarejea nyumbani baada ya siku ya mapumziko, siku chache tu kabla ya kufunguliwa kwa uwanja wa michezo Wa Disley hapo alhamisi mjini Shanghai.