China yazionya nchi mbali mbali dhidi ya kukiunga mkono chama cha Taiwan DPP

Rais wa China Xi Jinping akizungumza kwenye hafla kando ya mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) huko San Francisco, California Novemba 15, 2023. REUTERS

Wizara ya mambo ya nje ya China na balozi zake duniani kote mwishoni mwa wiki walizionya nchi mbali mbali dhidi ya kukiunga mkono chama cha Taiwan Democratic Progressive Party (DPP) na kulaani serikali za kigeni zinazompongeza rais mteule wa kisiwa hicho Lai Ching-te.

Baada ya mgombea urais wa chama cha DPP Lai kushinda uchaguzi siku ya Jumamosi, mawaziri na wanasiasa kadhaa kutoka nchi ambazo zina ushirikiano wa karibu na katika hali isiyo rasmi na kisiwa hicho kinachojitawala walituma salamu za pongezi kwa Lai na DPP.

Hii ilipelekea majibu ya haraka kutoka kwa balozi za China, zikiangazia kutofurahishwa kwa Beijing na nchi nyingine zinazoonekana kutoa uhalali kwa mgombea na chama cha siasa ambacho wao China wanakiona kama ni nguvu za kujitenga zikitumaini kuigeuza Taiwan, ambayo wanadai ni himaya yao, kuwa taifa huru.

Wizara ya mambo ya nje ya China siku ya Jumapili ilielezea taarifa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, iliyompongeza Lai na kusema Washington inatarajia kuendeleza uhusiano wake usio rasmi na Taiwan, ni sawa na kutuma ishara isiyo sahihi kwa vikosi vya kujitenga vya Taiwan.