China yatumia mabilioni kwa propaganda za kuibeba

China inamwaga mabilioni ya dola katika juhudi za kuunda upya mazingira ya habari ya kimataifa na kugeuza mtazamo wa mataifa mengi kwa manufaa ya Beijing, kwa mujibu wa tathimini mpya ya maafisa wa Marekani.

Ripoti iliyotolewa Alhamisi na kituo cha ushirikiano wa kimataifa cha wizara ya mambo ya nje ya Marekani, inashutumu serikali ya China kwa kutumia mbinu mchanganyiko katika adhma ya kuunda ulimwengu ambapo Beijing, itakuwa inadhibiti mtiririko wa habari muhimu kwa mbinu zote.

Imedai lengo la China ni kuunda mfumo wa ikolojia wa habari ambapo propaganda za China na habari potofu zitpata mvuto na kutawala.

Imeeleza bila kudhibitiwa, juhudi za jamhuri ya watu wa China, zitatengeneza upya mazingira ya habari ya kimataifa, na kujenga upendeleo na mapengo ambayo yanaweza hata kusababisha mataifa kufanya maamuzi ambayo yanaweka chini maslahi yao ya kiuchumi na usalama chini ya Beijing.