China yatakiwa kutoa ushirikiano zaidi wa Covid-19

Vyombo vya habari vya serikali nchini China, Jumanne vilipuuza ukubwa wa ongezeko la  maambukizo ya COVID-19.

Hayo yanatokea wakati wanasayansi wake wakitoa maelezo kwa shirika la Afya duniani (WHO), ambalo limekuwa likitafuta habari za kina juu ya mabadiliko ya virusi hivyo.

Chombo hicho cha kimataifa kiliwaalika wanasayansi kuwasilisha taarifa za kina juu ya mpangilio wa virusi kwenye mkutano wa kundi la kiufundi Jumanne, na imeitaka China kutoa taarifa juu ya watu kulazwa, vifo na chanjo.

WHO itawasilisha taarifa Jumatano, msemaji wake alisema baada ya mkutano na wanahabari.

Msemaji huyo hapo awali alisema shirika hilo lilitarajia majadiliano ya kina juu ya aina mpya ya virusi vinavyo sambaa China na ulimwenguni.

Kubadilika ghafla kwa China inavyo shughulikia Covid-19, kumekuwa kukichunguzwa sana nyumbani na nje ya nchi.