Hatua hii imekuja baada ya kuzungumza na mwenzake wa Russia mjini Beijing. Alisema China inalenga kuona vita vimesitishwa na kumalizika hivi karibuni.
Katika mkutano na Rais Xi Jinping wa China Jumanne, Lavarov alisema kuchaguliwa tena kwa Vladimir Putin kama Rais wa Russia kumehakikisha maendeleo zaidi ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Alishutumu "vikwazo visivyo halali" vilivyowekwa na Magharibi dhidi ya Russia na nchi nyingine.
Lavrov aliwasili Beijing Jumatatu ili kuonyesha ushirikiano na mshirika wa karibu wa kidiplomasia China. huku kukiwa na vita vikali vya Moscow dhidi ya Ukraine na juhudi zinazoendelea za kuoanisha sera zao za kigeni dhidi ya Marekani na washirika wake.