China yataka mkataba wa nyuklia wa Iran kushughulikiwa haraka

Rais wa China, Xi Jinping, Jumanne ametoa mwito wa kufanyika utatuzi wa mapema na sahihi, kuhusu suala la nyuklia ya Iran huku akielezea kuunga mkono jamuhuri hiyo ya Kislamu katika kusimamia haki na maslahi yake, kwa mujibu wa chombo cha habari cha China.

China itaendelea inaendelea kushiriki kwa kujenga, mazungumzo ya kuanzisha makubaliano ya kutekeleza makubali ya nyuklia ya Iran, rais Xi alimwambia rais wa Iran, Ebrahim Raisi katika mazungumzo yao mjini Beijing.

Makubaliano ya nyuklia yam waka 2015 yanadhibiti mpamgo wa uzalishaji uranium wa Iran kuwa vigumu kutengeneza silaha za nyuklia, kwa kubadilishana kwa kuondolewa vikwazo vya kimataifa.

Iran inasema imekuwa ikiendeleza zaidi nguvu za nyuklia kwa njia ya amani. Lakini 2018 aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trumop, aliachana na makubaliano hayo kwa kusema imefanya mengi kuzuia shuhuli za Iran za nyuklia, na kuiwekea vikwazo.