China imepoteza mshirika baada ya kujiuzulu kufuatia shinikizo, kwa Waziri Mkuu wa muda mrefu wa Bangladesh, Sheikh Hasina, ambaye wakati wa ziara ya Beijing mwezi uliopita alitia saini mikataba 28 ya nchi mbili na kukubali kuongeza uhusiano kati ya nchi hizo na kuwa ushirikiano wa kimkakati.
Jibu rasmi la Beijing kuhusu kukimbia kwa Waziri Mkuu halikuwekwa wazi na shirika la habari la Xinhua, lilipo nukuu Wizara ya Mambo ya Nje ikielezea Bangladesh kama jirani rafiki na matumaini ni kwamba utulivu utarejea haraka.
Lakini kwenye mitandao ya kijamii ya China, watu wamepongeza waziwazi ujasiri wa waandamanaji wa wanafunzi waliomuondoa Hasina, wakikabiliana na ukandamizaji mkali wa kijeshi ambao ulisababisha wanafunzi kadhaa kuuawa.