China yaomba kuhakikishiwa usalama wa raia wake waliyopo Pakistan

  • VOA News

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif (Kushoto), na bazozi wa China nchini humo Jiang Zaidong, wakizungumzia usalama wa raia wa China waliopo Pakistan. Picha ya Machi 26.2024.

Taarifa ya Jumanne imesema kuwa Pakistan imekubali kuimarisha usalama wa raia wa China pamoja na miradi ya China iliyopo kwenye taifa hilo la Kusini mwa Asia, wakati Beijing ikiomba hatua za haraka za kiusalama kuchukuliwa, kufuatia kuongezeka kwa tishio kutoka kwa wanamgambo.

China imewekeza mabilioni ya dola huko Pakistan katika miaka kadhaa iliyopita, wakati ikijenga miundomsingi chini ya mradi wa Reli na Barabara, huku pia ikiendesha bandari muhimu pamoja na mgodi muhimu nchini humo. Hata hivyo raia wa China pamoja na miradi yao wamekuwa wakishambuliwa na wanamgambo wanaopigania kile wanasema ni uporaji kwenye jimbo la kusini magharibi la Balochistan lenye utajiri mkubwa wa madini.

Taarifa hiyo imetolewa wakati wa ziara ya siku nne ya Waziri Mkuu wa China Li Quing, Jumatatu, ikiwa ya kwanza ya waziri mkuu wa China ndani ya miaka 11, siku chache tu baada ya shambulizi la kujitoa muhanga mjini Karachi kuuwa wahandisi wawili wa China, likiwa shambulizi la pili la aina hiyo mwaka huu. Taarifa kutoka wizara ya kigeni ya Pakistan imesisitiza azma ya serikali ya kuimarisha usalama nchini.