China yakosolewa kwa kupiga marufuku vitabu vya historia ya Mongolia

Picha katika maonyesho ya utamaduni barani Asia.

Wanaharakati wa utamaduni na lugha wa Mongolia wanasema kwamba amri ya serikali ya China ya kupiga marufuku baadhi ya vitabu vya historia ya Mongolia karibu miongo miwili baada ya kuchapishwa kwa mara ya kwanza, ni moja ya mifano ya ushawishi mkubwa wa China dhidi ya nchi hiyo.

Kuanzia maktaba hadi kinachofunzwa darasani, hatua zilizochukuliwa na mamlaka ndani ya Mongolia, eneo linalojitawala ndani ya China zinatia wasiwasi, wanaharakati na wataalam wameongeza.

Hatua hiyo inaonekana kama sehemu ya utawala wa China chini Xi Jinping kubuni utaifa wa China. Agosti 25 Shirika la kieneo la Inner Mongolia linalosambaza vitabu lilitoa ilani ikiagiza wanachama wake kusitisha usambazaji wa vitabu vyenye historia ya kabila la Mongolia, wakati wakihitajika kufuata historia kamili ya chama cha Kikomunisti cha China.