China yaimarisha ushawishi wake kwenye visiwa vya Solomons

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi (katikati) baada ya kuwasili Honiara, visiwa vya Solomons. May 26 2022

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi (katikati) baada ya kuwasili Honiara, visiwa vya Solomons. May 26 2022

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, akiwa na wajumbe 20, ameanza ziara kwenye visiwa vya Solomons.

Wang Yi atafanya ziara katika nchi nane, inayokuja wakati kuna hali ya wasiwasi kuhusiana na harakati za kijeshi na kifedha za Beijing katika kanda ya Pacific ya kusini.

China imesema kwamba ziara hiyo inazingatia historia yam da mrefu kuhusu urafiki kati ya Beijing na nchi hizo za visiwa.

Lakini Australia imejaribu kukabiliana na ziara hiyo kwa kutuma waziri wake wa mambo ya nje Penny Wong lwemue visiwa vya Fijji, kuonyesha uungaji wake mkono kwa Pacific.

Akiwa Fiji, Wong amesema kwamba ni uhuru wa kila nchi kuamua ushirikiano wake na mataifa mengine na mikataba wanayosaini, lakini akahimiza mataifa hayo kutathmini faida watakayopata wanaposhirikiana na Australia.