Mazoezi ya kijeshi ya China, karibu na Taiwan ambayo yameonekana kuwa ni ya kichokozi, yame-endelea Jumatatu licha ya kupangwa kumalizika.
Katika taarifa wizara ya ulinzi ya China imesema jeshi la ukombozi wa watu wa China katika komandi ya mashariki litajikita katika katika kukabiliana na nyambizi na makombora ya angani kwenye manuari karibu na Taiwan.
Haijawekwa wazi ni muda gani mazoezi yatafanyika ama yatajikita wapi.
China tayari imeshafanya mazoezi makali ya kijeshi ya siku nne katika maeneo sita kuzunguka Taiwan, ikiwa ni mwitikio wa ziara ya spika wa baraza la wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi aliyoifanya wiki iliyopita.
Pelosi ambaye ni mkosoaji wa China kwa kipindi kirefu, alitembelea Taiwan, Agosti 2 kuonyesha mshikamano na ungwaji mkono wa Marekani kwa kisiwa kinachojitawala.
China inaona ziara hiyo kama jambo lisilo kubalika na ukiukwaji wa sheria za himaya yake.