China yathibitisha kushiriki zoezila kijeshi huko South China Sea

Manowari ya kivita ya China katika mazoezi ya kijeshi mwaka huko South China Sea.

China imesema mazoezi ya kijeshi yalikuwa ya kawaida na yalifuata sheria zote za kimatiafa.

China imethibitisha Jumatatu kwamba manowari yake imeshiriki katika zoezi la kijeshi kwa mara ya kwanza wiki iliyopita katika eneo la South China Sea, siku chache baada ya maafisa wa serikali ya Taiwan inayojitawala kusema kwamba mazoezi hayo yako umbali wa kilomita 166 kusini mwa kisiwa hicho, kitendo kimeikasirisha China.

Mazoezi hayo ya kijeshi yalifanyika wakati kulipozuka utata mkubwa baada ya rais mteule wa Marekani, Donald Trump kuongea kwa simu na rais wa Taiwan,

Wizara ya Ulinzi ya China imesema meli yake ya kivita yenye kubeba ndege iliyotengenezwa na Russia pamoja na meli nyingine za kivita zilitia nanga katika eneo la pwani ya mashariki mwa Taiwan. China imesema mazoezi hayo yalikuwa ya kawaida na yalifuata sheria zote za kimataifa.

Jumatatu, ndege za kivita aina ya J-15 zilizokuwa zimebebwa ndani ya meli hiyo zilifanya mazoezi katika hali ya hewa isiyokuwa nzuri kwenye bahari hiyo,” kwa mujibu wa jeshi la majini la Ukombozi la Watu China. Meli hizo za kijeshi ziliendesha mazoezi ya helikopta za kivita katika maeneo yaliyokuwa hajaelezewa.