Honduras imeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China Jumapili baada ya kuvunja uhusiano na Taiwan, ambayo inazidi kutengwa na sasa inatambuliwa na mataifa 13 pekee.
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka China na Honduras walitia saini taarifa ya pamoja mjini Beijing, uamuzi ambao Wizara ya Mambo ya Nje ya China iliusifu na kuita chaguo sahihi.
Ushindi huo wa kidiplomasia wa China unakuja huku mivutano ikiongezeka kati ya Beijing na Marekani, kutokana kuongezeka uwezekano wa China kuelekea Taiwan inayojitawala yenyewe, na kuashiria kuongezeka ushawishi wa China, Amerika Kusini.
Uhusiano mpya wa China na Honduras umetangazwa baada ya serikali ya Honduras na Taiwan kutoa taarifa tofauti ya kuvunja uhusiano wao.
China na Taiwan zimekuwa zikipigania kutambuliwa kidiplomasia, huku China ikidai Taiwan ni sehemu ya himaya yake, na kutaka kuidhibiti kwa nguvu.