China itaondoa kwa muda malipo ya visa kwa raia wa Ufaransa, Ujerumani, Italy, Uholanzi, Uhispania na Malaysia wanapolitembea taifa hilo la pili lenye uchumi mkubwa duniani, ikiwa ni hatua ya hivi karibuni kuimarisha utalii baada ya kipindi cha janga la Covid.
Kuanzia tarehe 1 Disemba mwaka huu hadi Novemba 30 mwaka 2024, raia kutoka nchi hizo wanaoingia China kwa ajili ya biashara, utalii, kutembelea jamaa na marafiki, au kukaa kwa muda usiozidi siku 15 hawatahitaji visa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema Ijumaa.
China imekua ikichukua hatua katika miezi ya hivi karibuni, ikiwemo kufungua tena safari za ndege za kimataifa, kufufua sekta yake ya utalii kufuatia miaka mitatu ya hatua kali za kupambana na Covid 19 ambazo kwa kiasi kikubwa zilifunga mipaka yake kwa ulimwengu wa nje.