China inaendelea kuwavutia washirika wa Taiwan kwa kutumia mabilioni ya dola

Rais wa Honduras Xiomara Castro

Rais wa Honduras Xiomara Castro amewsili Shanghai leo Ijumaa, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu China ilipoanzisha upya uhusiano wake wa kidiplomasia na China, na kuachana na aliyekuwa mshirika wake wa karibu, Taiwan.

Castro anatarjiwa kukutana na rais wa China Xi Jinping kuweka mipango ya maendeleo ya baadaye kati ya nchi hizo mbili.

Shirika la habari la serikali ya China Xinhua, limeripoti kwamba Castro vile vile atahudhuria sherehe ya ufunguzi wa ubalozi wa Honduras mjini Beijing.

Honduras ilianzisha uhusino wa kidiplomasia na Chin mnamo mwezi March, na kuwa nchi ya hivi punde kumaliza ushirikiano wake wa kidiplomasia na Taiwan.

China inachukuliwa Taiwan, inayojitawala, kuwa mkoa wake, na inataka kurejesha kimabavu Taiwan chini ya utawala wake.

China imefanikiwa kushawishi nchi 9 kuacha kushirikiana na Taiwan, kwa kutumia uwekezaji wa mabilioni ya dola katika nchi hizo.