China bado yakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya COVID - 19

Picha ikionesha watu wakipima Covid China

Shirika la habari la Reuters limeandika leo Jumamosi. Hivi karibuni China ililegeza masharti ya kuzuiya kuenea kwa ugonjwa huo baada ya maandamano makubwa yaliyoenea katika maeneo mbalimbali ya nchi , wananchi wakidai kuchoshwa na masharti hayo.

Katika siku za karibuni inaenelezwa kwamba maambukizo ya ugonjwa huo ambao sasa unaenezwa na kirusi cha Omicron umepiga maeneo ya huduma nyingi ikiwemo za chakula na usambazaji wa mizigo.

Nyumba za kuhifadhia maiti na kuchoma katika mji huo wenye takriban watu milioni 22 zimeripoti kuwa na matukio mengi ya watu waliokufa kwa COVID kuliko ilivyokuwa awali.

Hata hivyo China haijatangaza rasmi idadi ya vifo kutokana na Covid tangu Desemba 7 wakati serikali ilipolegeza masharti yake ya sera ya Zero Covid ambayo ilihamasishwa sana na rais She Jimping .

Taasisi ya utafiti yenye makao yake Marekani imesema nchi hiyo inaweza kushuhudia kesi nyingi zaidi na watu zaidi ya milioni moja wanaweza kufa China kwa COVID mwaka 2023.

Kuongezeka kwa kasi ya vifo kutasababisha jaribio katika juhudi za mamlaka kuondoa China katika upimaji usio na mwisho, kufungwa kwa nchi, na masharti magumu ya usafiri na kuendana na ulimwengu ambao umefugunguliwa tena kuishi na ugonjwa huo.

Taarifa zinasema idadi rasmi ya kesi zimekuwa hazitolewi ipasavyo kutokana na kwamba kuna vipimo vichache vinavyofanyika kote nchini . Kumekuwa na mijadala kadhaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kukosekana kwa taarifa rasmi za idadi vifo na kesi Zitokanazo na COVID kwa takriban siku 10 .