Kampuni ya kutengeneza chanjo za Covid-19 ya BioNtech inalenga kuanza utengenezaji kwenye kiwanda chake cha chanjo cha mRNA chini Rwanda kufikia 2025, maafisa wake wamesema Jumatatu, ikiwa kampuni ya kwanza ya kigeni kutengeneza chanjo hizo barani Afrika.
Vifaa vya kwanza vya kutengeneza kiwanda hicho viliwasili mjini Kigali kwa makontena mwezi Machi, wakati vikianza kuunganishwa na kuunda mitambo inayojulikana kama BionNtainers.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mmoja wa waanzilishi wa kampuni hiyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu Ugur Sahin amesema kwamba kiwanda hicho kitaweza kutengenza kila aina ya chanjo za mRNA, akiongeza kupitia taarifa kwamba kampuni yake imetoa ufadhili wote wa kiwanda hicho kitakachogharimu dola milioni 150.
BioNTech imesema kwamba kiwanda hicho cha kwanza huenda katika miaka kadhaa ijayo kikapanuka na kuanza kwenye mataifa mengine ya Afrika maka vile Senegal na Afrka Kusini.