Chanjo ya Johnson & Johnson imeonyesha matokeo mazuri dhidi ya Corona

Mfano wa chanjo ya Johnson &Johnson (J&J)

Utafiti uliofanywa kutoka kati-kati ya mwezi Februari hadi Mei kwa zaidi ya wafanyakazi wa afya 470,000 ulionyesha matokeo mazuri kwa wale waliochanjwa na pia mdhibiti wa afya wan chi hiyo aliidhinisha chanjo moja ya Johnson & Johnson mwezi April

Chanjo ya Johnson & Johnson ya COVID-19 imekuwa na matokeo mazuri nchini Afrika kusini, mmoja wa wakuu wanaoendesha majaribio hayo Glenda Gray aliwaambia waandishi wa habari leo Ijumaa.

Utafiti uliofanywa kutoka kati-kati ya mwezi Februari hadi Mei kwa zaidi ya wafanyakazi wa afya 470,000 ulionyesha matokeo mazuri kwa wale waliochanjwa na pia mdhibiti wa afya wan chi hiyo aliidhinisha chanjo moja ya Johnson & Johnson mwezi April. Imekuwa inatumika pamoja na chanjo ya Pfizer.

Pia utafiti huo ulionyesha chanjo inazuia kifo kwa asilimia 91 hadi asilimia 92. Gray alisema na kwamba ina ufanisi wa asilimia 67 dhidi ya maambukizi wakati kirusi cha corona cha Beta kilipotawala na pia asilimia 71 wakati aina mpya ya kirusi cha Delta.

Kuanzia Alhamis zaidi ya watu milioni 8.3 walikuwa wamepewa chanjo nchini Afrika kusini. Ulimwenguni kote karibu watu bilioni 4.3 wamepata chanjo.