Kiongozi mkuu wa upinzani Zimbabwe, Nelson Chamisa amesema Jumamosi alikuwa na madai halali ya kuongoza taifa hilo baada ya kukataa uamuzi wa Mahakama ya Katiba ambayo ulimthibitisha Rais Emmerson Mnangagwa kama mshindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika Julai 30.
Chamisa alisema alikuwa na madai halali ya kuongoza taifa la Zimbabwe baada ya kukataa uamuzi wa mahakama ya katiba uliomthibitisha Mnangagwa ndiye mshindi wa kiti hicho.
Kulingana na taarifa ya shirika la habari la Reuters, Chamisa aliendelea kusema kwamba alishinda uchaguzi huo wa kwanza kufanyika tangu alipoondoka madarakani kiongozi wa muda mrefu nchini humo Robert Mugabe mwezi Novemba mwaka 2017.
Chamisa alidai kuwa Mahakama ya Katiba ilizuia juhudi zake alizotaka tume ya uchaguzi iwasilishe mahakamani ushahidi wote muhimu wa kusaidia kesi yake.
Mahakama ilitupilia mbali siku ya Ijumaa madai ya Chamisa ikisema alishindwa kuthibitisha shutma za wizi wa kura.