CDC Marekani kutoa waraka kuhusu aina mpya ya kirusi cha Delta

Nembo ya taasisi ya kuzuia na kudhibiti magonjwa (CDC) Marekani

Waraka huo unawasihi  maafisa wa CDC kuandaa ujumbe wa umma ambao utasisitiza  njia bora zaidi kwa chanjo ya kujikinga dhidi virusi hivyo vinavyoambukiza kwa kasi ambavyo ni tofauti kabisa na virusi vingine  na vinasambaa zaidi kuliko kirusi cha Ebola au cha mafua ya kawaida

Kulingana na ripoti katika magazeti ya Washington Post na New York Times, nchini Marekani leo Ijumaa kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) Marekani kinatarajiwa kutoa hadharani waraka wa ndani kuhusu afya kwa aina mpya ya kirusi cha corona cha Delta ambacho kinaweza kusambaa kwa haraka sana kama tetekuwanga kwa watu waliochanjwa na wasiochanjwa.

Magazeti hayo yaliripoti kuwa waraka huo ulisambazwa kwa maafisa wa CDC. Maelezo yake yanabainisha ugumu wanaopata maafisa katika kuwashawishi baadhi ya watu kupatiwa chanjo na kuvaa barakoa.

Raia wa kawaida akifuata muongozo wa CDC dhidi ya COVID-19

Waraka huo unawasihi maafisa wa CDC kuandaa ujumbe wa umma ambao utasisitiza njia bora zaidi kwa chanjo ya kujikinga dhidi virusi hivyo vinavyoambukiza kwa kasi ambavyo ni tofauti kabisa na virusi vingine na vinasambaa zaidi kuliko kirusi cha Ebola au cha mafua ya kawaida.

Pamoja na aina mpya ya kirusi cha Delta ambacho kinasababisha COVID-19 kusambaa kwa haraka Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza wafanyakazi wa serikali kuu lazima wapewe chanjo au wapimwe mara kwa mara pamoja na kuvaa barakoa.